Watu wanne wafariki katika ghasia India

0
34


 

India. Watu wanne wamefariki dunia kufuatia mapambano ya risasi kati ya wafuasi wa chama tawala cha mlengo wa kulia nchini humo na upande pinzani.

Mauaji hayo yalitokea leo Jumapili June 9, katika jimbo la Bengal Magharibi huku wengine 18 wakijeruhiwa.

Polisi nchini India wamesema jimbo hilo limekuwa na hali tete tangu chama Bharatiya Janata- BJP cha Waziri Mkuu, Narendra Modi kuzindua kampeni ya kishari kwa lengo la kushinda viti vya ubunge mwishoni mwa mwaka jana.

Afisa mmoja wa polisi ameliambia Shirika la Habari la AFP kuwa watu watatu kati ya waliofariki ni wafanyikazi wa chama hicho cha BJP na mmoja alikuwa mfuasi wa chama cha eneo hilo cha Trinamool.

Ghasia ziliongezeka katika jimbo hilo wakati wa uchaguzi mkuu ulioandaliwa kati ya Aprili na Mei ambako zimeendelea hata baada ya matokeo kutangazwa na kukipa chama cha BJP ushindi mkubwa kitaifa

 

Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here