Wanawake wenye watoto wengi Nchini Hungary kusamehewa kodi

0
64


Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Wanawake wenye watoto wanne na zaidi kusamehewa kodi Hungary

Wanawake nchini Hungary wenye watoto wanne na zaidi watasamehewa kulipa kodi ya mapato maishani mwao.

Waziri mkuu wa nchi hiyo Viktor Orban ameyasema hayo wakati akizindua mipango iliyobuniwa kwa ajili ya kuongeza idadi ya watoto wanaozaliwa.

Amesema hiyo ni njia ya kulinda mustakabali wa Hungary bila ya kutegemea Wahamiaji.

Katika hatua hizo zinazochukuliwa pia, wanandoa vijana watakuwa wanapewa mkopo usio na roba wa dola elfu 26, ambao utafutwa watakapofikisha watoto watatu.

  • Idadi ya watoto wanaozaliwa duniani imepungua
  • Je akina mama wanastahili kustaafu mapema?

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

Waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban

Wanasiasa wa mrengo wa kulia nchini humo wamekuwa wakipinga uhamiaji unaofanywa na Waislamu.

Idadi ya watu nchini Hungary imekuwa ikipungua kwa elfu 32 kwa mwaka na wanawake nchini humo wana watoto wachache kushinda wastani wa Umoja wa Ulaya.Waziri mkuu huyo wa Hungury amesema kwa nchi za magharibi jibu la kupungua kwa watoto wanaozaliwa kwa Ulaya ni Wahamiaji. ”…kwa kila mtoto anayepungua lazima mwengine aje, halafu idadi itakuwa sawa…Watu wa Hungary wanafikiri tofauti, hatuhitaji idadi tunataka watoto wa Hungary…” alisema.

Waziri Mkuu huyo wa Hungary amekuwa akichukua hatua kali dhidi ya wahamiaji, hali ambayo mara kwa matra imefanya kutofautiana na wenzake wa Ulaya.

Ufaransa ni nchi inayoongoza kwa mwanamke kuzaa watoto wengi nchi za Umoja wa Ulaya kwa wastani wa 1.96 huku Hispania ikiwa na kiwango cha chini kabisa cha 1.33.

Niger nchi iliyoko Afrika magharibi ndiyo inayoongoza kwa mwananmke kuzaa watoto wengi duniani kwa watoto 7.24 kwa mwanamke mmoja.Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here