Waalgeria wanamtaka Bouteflika ajiuzulu licha ya upigaji kura kuchelewa

0
19


Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Waandamanaji wa Waalgeria wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa maandishi ya kiarabu “hakuna mbadala zaidi ya kuondoka””

Maelfu ya waandamanaji wamekusanyika katika mji mkuu wa Algeriakudai kuachia mamlaka mara moja kwa rais wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika licha ya kutangaza kuwa hana nia ya kugombea tena kiti hicho kwa muhula mwingine.

Jumatatu ,aliahirisha uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika tarehe 18 Aprili.

Waandamanaji hata hivyo ,wanamshutumu rais huyo mwenye umri wa miaka 82-kwa kurefusha zaidi muhula wake kinyume cha sheria.

Wanafunzi wamekuwa wakiongoza maandamano makubwa dhidi ya Bouteflika ambayo yameingia siku ya tano sasa.

Rais huyo ambaye ni mgonjwa huonekana kwa nadra sana hadharani na hajawahi kuhutubia umma tangu alipopata kiharusi mwaka2013.

Alirejea nchini mwaka mapema wiki hii baada ya kulazwa katika hospitali nchini Uswiss

Nusu ya raia wa Algeria wanachini ya umri wa miaka 30 na kiwango cha ukosefu wa ajira kimechochea hasira dhidi ya serikali.

Kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya Noueddine Bedoui na mipango ya kuundwa kwa serikali ya mseto kumeshindwa kuzima maandamano.

Waandamanaji wanataka nini?

Wamepuuzilia mbali mpango wa Bwana Bedoui wa kuunda serikali ya watekelezaji itakayowajumuisha Waalgeria vijana.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Waandamanaji wanamshutumu rais huyo mwenye umri wa miaka 82-kwa kurefusha zaidi muhula wake kinyume cha sheria

Alisema katika kikao chake cha kwanza na waandishi wa habari siku ya Alhamisi kuwa, serikali mpya itakuwa na mamlaka kwa muda mfupi tu na akawataka wapinzani kushirika katika mazungumzo chanya.

Lakini wanaharakati wamekwisha kwamba hawataki mashauriano kwa sasa.

Tangazo la Bouteflika la Jumatatu la kwamba ameacha mpango wake wa kugombea tena kwenye uchaguzi ambao utarefusha muda wa utawala wake wa miaka 20, awali lilipokelewa kwa shangwe kubwa,lakini wanaharakati sasa wanauona kama njama za chama tawala cha National Liberation Front za kuendelea kung’ang’ania madaraka.

  • Abdelaziz Bouteflika:Rais asiyezungumza

Waandamaji wa siku ya Ijumaa wamekusanyika katika medani ya Grand Poste square na pia wamekuwa wakimpinga rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambaye amekua akitoa wito wa kuwepo kwa kipindi cha mpito cha maana.

“Macron, nenda huko” walipaza sauti, huku wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa maneno hayo.

Nini kitakachofuata?

Mazungumzo yamepangwa kufanyika kwa ajili ya mashauriano ya hali ya hali ya baadae ya kisiasa nchini Algeria , ambayo yataongozwa na mwanadiplomasia wa zamani wa Umoja wa Mataifa Lakhdar Brahimi.

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

Maandamano yamekuwa yakiongozwa na vijana wa Algeria wanaosema serikali haishikiki

Mkutano ambao bado tarehe yake haijapangwa, utalenga kuangalia kipindi cha mpito cha kisiasa , kuandaa muswada wa katiba mpya na kutangaza tarehe ya uchaguzi.

Bwana Brahimi, ambaye alikuwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa nchi za kiarabu kwa ajili ya Syria hadi tarehe 14 Mei 2014, alikutana na rais jumatatu ambapo alisema ni muhimu “kuugeuza mzozo huu kuwa mchakato unaojenga”.

Jeshi la Algeria linatarajiwa kuwa na nafasi muhimu katika kipindi cha mpito.

Waandamanaji na washiriki katika vita vya kupigania uhuru wa nchi hiyo vya kati ya mwaka 1954-1962 pia watakuwa miongoni mwa wawakili katika mkutano huo wa kitaifa



Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here