Video ya ‘Ni Wewe’ yafikisha views mil. 1, Ommy Dimpoz amtumia salamu Steve Nyerere ‘nakuheshimu, najua kuna kitu umejifunza’

0
65


Video ya wimbo mpya wa ‘Ni Wewe’ wa Ommy Dimpoz imefikisha views milioni 1 kwenye mtandao wa YouTube ndani ya siku nne tangu kichupa hicho kiachiwe.

Ommy Dimpoz ametumia nafasi hiyo kumjibu mchekeshaji, Steve Nyerere ambaye siku ya jana alimuomba radhi kwa kauli yake ya ‘Ommy Hatoimba tena’ .

Thank you for the Love & Support 1 Mil viewers in 4 days kwangu ni wengi sanaaaa ukizingatia December yote ilinikuta Kitandani wala sikuwa na matarajio kama nitasimama tena pia stress na mawazo ukiona wasanii wenzako wako busy na msimu wa Sikukuu kuingiza chochote.Lakini nilimshukuru Mungu Maana yeye ndo Anayepanga na Sikuchoka kumuomba Naimani Afya yangu itaendelea kuimarika zaidi na Zaidi Inshaallaah,“ameandika Ommy Dimpoz kwenye ukurasa wake wa Instagram na kutolea ufafanuzi kuhusu ombi la msamaha la Steve Nyerere.

Kuhusu my Brother TIVU AKE 🤣 @stevenyerere2Mimi kama nilivyosema Mwanzo sina kinyongo na Wewe najua kama binadamu uliteleza na kuna kitu umejifunza na ningependa utambue bado nakuheshimu sana si unajua wewe ndo kiongozi wetu kwenye Mambo yetu yale 😜🤣🤣 sasa hivi Konseksheni Yangu kubwa ni Afya mkubwa mengine tusahau sawa🤣 halafu kuhusu hizi clip niache tu nipost maana zinachekesha halafu ntakuwa nawasapot wachekeshaji wenzako,“ameandika Ommy Dimpoz.

Wimbo wa Ni Wewe ni wimbo ambao Ommy Dimpoz ameelezea namna alivyopitia magumu kipindi anaugua, na kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kumfikisha hapa alipo.

Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here