Utalii Uganda: Shutuma kali dhidi ya kutumia umbo la wanawake kama kivutio Uganda

0
50


Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Waziri wa utalii nchini Uganda Godfrey Kiwanda , anaamini wanawake wanene ama wanono wanaweza kuwavutia watalii nchini humo

Waziri wa utalii nchini Uganda amependekeza kuwe na onyesho la wanawake wenye maumbo makubwa ili kuvutia wageni zaidi wanaoitembelea nchi hiyo.

Godfrey Kiwanda alielezea mpango huo wakati wa uzinduzi wa ukurasa wa pamoja, Miss Curvy Uganda,katika mji mkuu Kampala.

Akinyoosha mkono wake kwa washiriki wa zoezi hiko alisema kuwa, alisema kuwa wanawake wote wanaojumuisha walikuwa “hadithi tunayouza” kwa wageni.

  • Je ukeketaji ni nini, unafanyika wapi na kwa nini?
  • Viwango vya elimu Uganda na Tanzania vyashuka

Maoni ya Mr Kiwanda yametajwa kama “udhalili” na “kudhalilisha”, na kumeanzishwa harakati nchini Uganda ili kupata mpango ingawa mpango huo umepingwa.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

mitandao ya kijamii ikatibuliwa na jumbe zenye kukinza wazo bunifu hilo

Akizungumza katika uzinduzi wa kivutio hicho mapema wiki hii , waziri huyo alisema kuwa itakuwa “tukio la kipekee ambalo litawaonesha mabanati wakionesha maumbo yao mazuri yaliyo nona”

“Tumepewa uwezo wa kawaida, wanawake wenye kutazamika ambao wana mvuto machoni kuangalia,” tovuti ya habari ya Uganda ya Daily Monitor ilimnukuu akisema. “Kwa nini hatutumii watu hawa kama mkakati wa kukuza sekta yetu ya utalii nchini Uganda?”

  1. Je vijana Uganda wana uraibu wa mchezo wa kamari?
  2. Bobi Wine aendelea kuitikisa Uganda
  3. Viwango vya elimu Uganda na Tanzania vyashuka

Kauli hiyo haikupokelewa vyema nchini humo hasa kwenye mitandao ya kijamii kulichafuka ujumbe wa aina kwa aina Bila shaka, kulikuwa na sintofahamu katika mchakato wa kukuza sekta ya utalii nchini humo na wanaharakati wa kutetea haki za wanawake, ama wanawake wenyewe walionona nao walifurukutwa kutoa maoni yao.

Watu wengine walimshutumu bwana Kiwanda kwa kuzungumza juu ya wanawake wanono kama kwamba walikuwa kama wanyama walioko katika bustani ya wanyama, na mwanamke mmoja alihoji kama ingewezekana basi wawekwe bustanini ili watazamwe kama wanayama watendewavyo “.Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here