Tundu Lissu kufungua shauri kudai stahiki zake zilizositishwa

0
21


Haki miliki ya picha
TUNDU LISSU

Image caption

Mbunge wa Singida Tundu Lissu kudai stahiki zake mahakamani

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amesema amewaelekeza mawakili wake nchini Tanzania, kuanza mchakato wa kufungua mashauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania, ili kudai uongozi wa Bunge urejeshe stahili zake zote zilizozuiliwa, nakulizuia lisiziingilie au kuziathiri tena kwa namna nyingine yoyote.

Lissu amesema uamuzi wa kumfutia mshahara na posho za kibunge ambazo kila Mbunge hulipwa, awe anaumwa au mzima, awe amehudhuria vikao vya Bunge au hajahudhuria, ni uthibitisho mwingine wa ukiukaji wa Katiba, Sheria na taratibu.

Mshahara wa Tundu Lissu waingia mashakani

Marufuku kuingia na kucha,kope bandia Bungeni Tanzania

Katika waraka wake alioutoa kwa njia ya picha ya video akiwa nchini Ubelgiji alisema”Uamuzi wa Bunge kunifutia mshahara na posho zangu ulifanyika kabla hata ya Spika Ndugai kuombwa, na kutoa,mwongozo huo. Ndio kusema kwamba Bunge la Spika Ndugai na Katibu wa Bunge Kagaigai limezuia mshahara na posho za kibunge tangu mwezi Januari”alieleza Lissu.

Hatua hii imekuja baada ya mwezi uliopita Mbunge wa Geita vijijini Joseph Msukuma kutoa hoja bungeni kuhoji uhalali wa Tundu Lissu kuendelea kupata mshara huku akiwa hahudhurii vikao kwa sababu ambazo hazijulikani.

”Kwa kuwa zipo sheria zinazoruhusu mtu kuitwa mgonjwa tunaona mheshimiwa Tundu lissu anazunguka kwenye nchi mbalimbali lakini huku anasomeka kama mgonjwa sasa mheshimiwa spika nilikua naomba muongozo wako ni lini Bunge litasitisha mshahara wake kwa kuwa ameshapona anazurura na bunge linaendelea na yeye hayupo na mnaendelea kumlipa mshahara na anazunguka nje anatukana bunge ,anatukana viongozi”.Alisema mbunge Msukuma

Akijibu hoja hiyo Spika Job Ndugai alikubaliana na hoja hiyo akiahidi kufanyia kazi.

Image caption

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai akiendesha kikao cha Bunge

”Ni kweli jambo hili la Tundu Antipas Lissu linahitaji kuangaliwa kipekee kwa maana ya kwamba mbunge hayupo jimboni kwake, hayuko hapa bungeni, hayupo hospitalini, hayupo Tanzania na taarifa zake Spika hana kabisa wala hajishughulishi kumuandikia Spika kumwambia niko mahali fulani au nafanya hivi na kama ni mgonjwa hakuna taarifa yeyote ya daktari halafu unaendelea kumlipa malipo mbalimbali nadhani hoja yako ni ya msingi kuwa iko haja ya kusimamisha malipo ya aina yeyote ile mpaka hapo ambapo tutakapopata taarifa kuwa yuko wapi na anafanya nini”.Alisema Ndugai

Lissu amesema kuwa mshahara na posho za kibunge ambazo kila Mbunge hulipwa kila mwezi sio fadhila bali ni haki ya kikatiba na kisheria ya kila mbunge wa Tanzania.

Aidha, haki hiyo haitegemei utashi binafsi wa Spika Ndugai na Katibu wa Bunge.Vile vile, haki hii haiwezi kufutwa ama kusimamishwa kwa sababu ya mbunge kutohudhuria vikao vya Bunge au kwa sababu nyingine yoyote.

”Nje ya Katiba na Sheria ya Uendeshaji wa Bunge, namna pekee ambayo mshahara na posho za kibunge unaweza kuathiriwa kihalali ni kwa Mbunge kusimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao vya Bunge kwa kukiuka maadili ya Bunge”.AlielezaSource link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here