Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 11.02.2019: Solskjaer, Almiron, Schmeichel, Fred, de Ligt

0
78


Haki miliki ya picha
PA

Ole Gunnar Solskjaer anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha wa kudumu wa klabu ya Manchester United – lakini klabu hiyo inatazamiwa kusubiri mpaka mwisho wa msimu ili kutoa tangazo hilo. (Sun)

Kocha Rafael Benitez amempigia chapuo kiungo rai wa Paraguay Miguel Almiron, 25, tkuwa atafanya vyema klabuni hapo mara baada ya kuvunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo. (Guardian)

Peter Schmeichel amedai kuwa mtoto wake ambaye ni kipa wa Leicester City Kasper, 32, anapanga kuihama klabu hiyo kwa kuwa hana furaha ya Maisha chini ya kocha Claude Puel. (Sun)

  • ‘Kombe la EPL si letu msimu huu’
  • Tetesi za soka Ulaya Jumapili 10.02.2019

Wolves ndiyo vinara katika mbio za kumsajili kinda raia wa Ureno Joao Felix, 19, na tayari kocha Nuno Espirito Santo kameeleza nia ya kumtaka kiungo huyo wa Benfica. (Mirror)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Joao Felix

Solskjaer amemuhakikishia kiungo raia wa Brazil Fred, 25, kuwa yupo kwenye mipango yake, baada ya kumng’oa kumuondoa kwenye kikosi kilichoivaa Fulham mwishoni mwa wiki. (Manchester Evening News)

Chelsea watataka kupewa mchezaji raia wa Ivory Coast iFranck Kessie, 22, endapo AC Milan watataka kumsajili moja kwa moja kwa moja kiungo wake raia wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 24. (Daily Star)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Tiemoue Bakayoko

Kocha wa Crystal Palace Roy Hodgson yupo tayari kumpa ushauri kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate ili kumjumuisha kikosini beki Aaron Wan-Bissaka, 21. (Independent)

Wachezaji wa Manchester City raia wa Ureno kiungo Bernardo Silva, 24, na beki Mfaransa Aymeric Laporte, 24, wameongeza thamani zao za usajili maradufu baada ya kuwa na msimu mzuri klabuni hapo. (CIES Football via Manchester Evening News)

  • Cavani na Neymar kukosa mechi dhidi ya Man Utd

Juventus wanadaiwa kuongoza mbio za kutaka kumsajili beki kinda wa klabu ya Ajax ya Uholanzi Matthijs de Ligt, ijapokuwa Barcelona, Manchester City na Liverpool woye pia wanammezea mate mchezaji huyo mwenye miaka 19.

Haki miliki ya picha
Soccrates Images

Image caption

Matthijs de Ligt (kushoto) nawaniwa na Juventus, Barcelona, Man City na Liverpool

Beki wa pembeni raia wa Ufaransa Faitout Maouassa, 20, hakuwa tayari kujiunga na klabu ya Newcastle mwezi uliopita lakini amesema ni ndoto yake kuchezea Ligi ya Premia siku moja. (L’Equipe via Newcastle Chronicle)

Miamba hiyo ya Serie A wanatarajiwa kufanya mazungumzo na kiungo wa Real Madrid Isco, 26, ama kiungo raia wa Colombia James Rodriguez, 27 – ambaye kwa sasa anakipiga kwa mkopo na Munichfrom Real – ili kuziba pengo la mshambuliaji raia wa Argentina forward Paulo Dybala, 25, endapo atahama klabu hiyo mwishoni mwa msimu. (Tuttosport)Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here