Straika mpya Simba ni huyu

0
42


 

By THOBIAS SEBASTIAN

KIKOSI cha mabingwa wa Ligi Kuu Bara Simba kabla ya msimu kumalizika walikuwa wakihusishwa kuwanasa washambuliaji watano kutoka katika nchi mbalimbali ili kuja kuongeza nguvu katika kikosi hiko msimu ujao.
Washambuliaji hao ambao Simba walikuwa wakihusishwa nao ni Jacques Tuyisenge kutokea Gor Mahia ya Kenya, Lazadius Kambole wa Zesco United ya Zambia, Yacouba Songne wa Asante Kotoko ya Ghana, Walter Nkana ya Zambia na Juan Makusu wa AS Vita.
Ofisa Mtendaji mkuu wa Simba Crescentius Magori alisema kuhusu kuhusishwa na baadhi ya wachezaji kutoka katika timu mbalimbali si jambo la kushangwazwa haswa kwenye kipindi kama hiki cha usajili lakini timu yao itafanya usajili kulingana na mapungufu ambayo yalijitokeza msimu.
Magori alisema mshambuliaji kama Tuyisenge vile ambavyo anacheza nao John Bocco na Meddie Kagere ambao wanacheza kama yeye kwahiyo ni vigumu kumsajili lakini kuna ulazima wa kuongeza mshambuliji lakini kwa sifa nyingine ambazo tunazitaka.
“Mshambuliaji ambaye tunamtaka ni yule ambaye anaweza kucheza akitokea pembeni kama winga, mwenye spidi, anaweza kupiga huku akiwa kwenye mwendo lakini msumbufu kwa mabeki wa timu pinzani na ikipatikana nafasi hata moja aweze kuitumia,” alisema.
“Aina ya mshambuliaji mwenye sifa hizo ndio tutaenda kumsajili kwani tumeingia katika soka na tunamtafuta na kama tutafanikiwa kumpata kwa gharama yoyote ile tutamuongeza katika timu yetu kwa maana ya kumsajili,” alisema Magori.

Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here