Shambulio katika misikiti ya Christchurch: Watu 40 wameuawa katika shambulio la kigaidi New Zealand

0
18


Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Emergency services personnel transport a person on a stretcher

Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern anasema watu 40 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa vibaya baada ya kuzuka mashambulio katika msikiti miwili katika mji wa Christchurch, huko New Zealand.

Waziri mkuu huyo amelitaja shambulio hilo kuwa mojawapo lililotanda ‘kiza kikubwa’ siku ya leo nchini humo.

Wanaume watatu na mwanamke mmoja wamekamatwa, kamishna wa polisi Mike Bush anasema, lakini ameonya kwamba huenda washukiwa zaidi wapo.

Inaarifiwa kwamba washambuliaji hao hawakuwa kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa lakini ni wazi kwamba wana itikadi kali.

Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison amesema mojawapo ya waliokamatwa ni raia wa Australia.

Amemtaja mshukiwa wa shambulio hilo kuwa “gaidi mwenye itikadi kali za mrengo wa kulia”.

Walioshuhudia mkasa huo wameambia vyombo vya habari kwamba walilazimika kutoroka kuokoa maisha yao na waliona watu walioanguka chini wanaovuja damu nje ya mskiti wa Al Noor mosque.

Police inasisitiza kwamba hali bado haijaimarika na wamethibitisha pia kwamba “vilipuzi kadhaa vilivyofungwa kwenye gari vimeharibiwa”.

Maafisa wameshauri misikiti yote katika mji huo ifungwe mpaka ilani itakapotolea, wakieleza kwamba hili lilikuwa shambulio la ghasia ambalo halikutarajiwa.

  • Rwanda yapiga marufuku ndege za Boeing 737 Max katika anga yake
  • ‘Kimbunga kibaya’ kuwahi kushuhudiwa kimetua Msumbiji

Mohan Ibrahim, ambaye alikuwa katika eneo hilo la msikiti wa Al Noor ameliambia gazeti la Herald: “Awali tuliona ni hitilafu zaumeme lakini mara tu watu wote wakaanza kutoroka.

“Bado rafiki zangu wamo ndani. Nahofia usalama wa maisha ya rafiki zangu.”

Haki miliki ya picha
Google

Nini kilichofanyika katika mskiti?

Bado haijulikani wazi nini kilichofanyika ndani ya misikti hiyo, taarifa mpaka sasa zimetoka kwa walioshuhudia mkasa na waliozungumzana vyombo vya habari.

Mashahidi wametaja kuona watu wakiwa wameanguka chini wanavuja damu.

Inaarifiwa mshambuliaji alilengas ehemu ya maombi ya wanaume, na baadaye kuelekea katika sehemu ya wanawake.

Watu wamehamishwa pia kutoka msikiti wa pili katika kitongoji cha Linwood na kamishna w apolisi amesema “watu kadhaa wameuawa ” katika maenoe mawili.Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here