Real Madrid: Kuwasili kwa Eden Hazard na wengine kunaashiria kikosi kipya cha Galacticos

0
27


Real Madrid, the Galacticos.

Katika miongo kadhaa iliopita , mabingwa hao wa Uhispania wamejipatia umaarufu wa matumizi ya hali ya juu kuwanunua wachezaji.

Kutoka Luis Figo na David Bekcham hadi Christiano Ronaldo na Gareth Bale, rais wa klabu hiyo Florentino Perez hajuitii matumizi anayofanya ili kuwakusanya wachezaji nyota duniani.

Katika miaka ya hivi karibuni, hatahivyo mtazamo huo umesahaulika.

Mbali na kuwasili kwa Thibaut Courtois kutoka Chelsea msimu uliokwisha, Real haijajihusisha na usajili wa mchezaji nyota tangu 2014 wakati Toni Kross na James Rodriguez walisajiliwa.

Tangu wakati huo, wakufunzi waliofuata kama vile Carlo Ancelotti , Rafale Benitez , Zinedine Zidane, Julen Lopetegui , Santi Solari na sasa Zidane tena- wamekuwa wakiwashirikisha wachezai wale wale kama vile Keylor Navas, Sergio Ramos, Raphael Varane, Dani Carvajal, Marcelo. Kross, Casemiro, Luka Modric, Isco, Bale, Ronaldo na Karim Benzima wakiwa wakitegemewa pakubwa na timu hiyo mwaka baada ya mwaka.

Kwa nini mabadiliko hayo ya sera? je wachezaji wapya ni akina nani?, je kutakuwa na wengine zaidi? na je hilo linamaanisha nini kwa nyota waliohudumu kwa kipindi kirefu?

Hatimaye Zidane amshawishi Perez.

Muda tu baada ya kuishinda Liverpool mnamo mwezi Mei 2018 na kuibuka mshindi wa kombe la mabingwa Ulaya kwa msimu wa tatu mfululizo, Zidane alichukua hatua isio ya kawaida – alijiuzulu, akidai kwamba hawezi kupata mafanikio na raslimali alizonazo.

Zidane amekuwa akisema kwamba mafanikio katika ligi ya nyumbani ni thibitisho zuri la uwezo wa timu na alihisi ushindi wa kombe la ligi ya mabingwa 2018 ulikuwa unaashiria kushuka kwa kiwango cha klabu hiyo swala ambalo lilijitokeza wakati ilipomaliza katika nafasi ya tatu msimu huu.

Tayari kulikua na ishara mbaya baada ya kuuzwa kwa Ronaldo, na Zidane alikuwa akituma ujumbe kwamba iwapo asingewezeshwa kufanya mabadiliko aliotaka ilikuwa wakati wa kuondoka.

Wiki chache tu baada ya Zidane kujiuzulu , ilionekana wazi kwamba alikuwa sawa.

Baada ya Lopetegui na Solari waliohudumu kwa wiki chache katika klabu hiyo , Perez alirudi kwa Zidane na mkia katikati ya miguu yake, akikubali maono yake kwamba kikosi hicho kilihitaji kufanyiwa mabadiliko.

Zidanae alirudi nyuma na kukubali lakini kwa masharti.

Hazard ndiye anayeongoza kikosi hicho kwa sasa

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Real wamewasjili Rodrygo (Santos), Eder Militao (Porto), Luka Jovic (Eintracht Frankfurt) na Ferland Mendy (Lyon) msimu huu

Kiungo muhimu cha mabadili ya Real Madrid, msimu ujao ni usajili wa Eden Hazard.

Rais huyo wa Ubelgiji alifuatiliwa kwa kipindi cha mwaka mmoja na Perez na kuvutia mashabiki 50,000 katika uwanja wa Bernabeu wakati alipozinduliwa.

Huku akiuzwa kwa dau la Yuro milioni 100 , mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea atajiunga na mshambuliaji Benzema.

Lakini Hazard siye mchezaji wa pekee katika safu ya mashambulizi huku Real pia ikimsajili nyota mwenye talanta inayozidi kuimraika, Luka Jovic.

Mchezaji huyo wa Serbia 21 ameifungia magoli 27 Eintracht Frankfurt msimu uliopita na anatarajiwa kuhusishwa katika kikosi cha kwanza baada ya kununuliwa kwa dau la Yuro 60m.

Mchezaji mwengine aliyesajiliwa ni beki wa kushoto Ferland Mendy ambaye amejipatia umaarufu mkubwa wakati wa kampeni ya Lyon msimu uliopita na anatarajiwa kushindana na mchezaji wa nyumbani Sergio Reguilon katika upande wa kulia ili kumrithi Mercelo.

Huku nahodha Ramos akiwa na umri wa miaka 33 , beki wa kati wa siku za usoni tayari amepatikana kupitia kuwasili kwa Eder Militao kwa dau la Yuro milioni 50 kutoka Porto huku mchezaji wa mwisho kusajiliwa akiwa winga Rodrygo Goes kutoka klabu ya Santos mwenye umri wa miaka 18 akitajwa kuwa uwekezaji wa siku zijazo.

Na usajili huo sio wa mwisho. Walipokuwa wakisubiri kuwasili kwa Hazard katika uzinduzi wake siku ya Alhamisi , mashabiki wa Real walijifurahisha wakisema: Twamtaka Mbappe” na haijulikani iwapo mchezaji huyo wa Ufaransa – ambaye hivi karibuni alikiri kwamba hajui kitakachotokea kuhusu hatma yake -ataondoka PSG katika miezi michache ijayo.

Uvumi unaomuhusisha Zidane na nyota mwingine wa Man United Paul Pogba hautaki kuisha, huku kiungo wa kati wa Lyon Tanguy Ndombele akichukuliwa kama mchezaji atakayenunuliwa iwapo Pogba hatoruhusiwa kujiunga na klabu hiyo.

Wachezaji wanaoondoka: Bale, James na Asensio?

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Bale na Asensio walikuwa ndani na nje msimu uliopita

Usajili wa wachezaji wa hivi karibuni , pamoja na kurudi kwa baadhi ya wachezaji waliotolewa kwa mkopo umeongeza idadi ya wachezaji wa kikosi cha Zidane hadi kufikia 37, na kifedha ni wazi kwamba baadhi yao watalazimika kuuzwa ili kuleta mapato.

Mapato madago ya kati ya Yuro milioni 10-20 kwa wachezaji kama vile Dani Ceballos, Marcos Lliorente , Theo Hernandez na Mariano Diaz yanaweza kulipa fedha alizonunuliwa Hazard mbali na kutoa nafasi katika kikosi hicho.

Lakini baadhi ya wachezaji nyota pia watauzwa kuanzia Gareth Bale.

Winga huyo wa Wales hana uhusiano mzuri na Zidane hivyobasi hatua ya kumtafutia klabu nyengine mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham ni mpango uliopo – kufikia sasa , hatahivyo, uwezo wa kumuondoa mchezaji huyo mwenye majeraha yasioisha pamoja na mshahara mkubwa uko juu.

Maamuzi kama hayo pia yanamuandama kiungo wa kati wa Colombia James Rodrigues ambaye hatakiwi na Zidane na kwamba hakuimarika wakati wa mkopo wake katika klabu ya Bayern Munich ili kuweza kusalia

Marcelo na Navas pia huenda wakaondoka iwapo ombi zuri litawasilishwa huku hatma ya Isco ikiwa haijulikani licha ya uhusiano wake wa karibu na Zidane huku mchezaji mwengine mwenye talanta akiwa mshambuliaji Marco Asensio ambaye hajaimarika zaidi ya ilivyotarajiwa.Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here