RC Mtwara aagiza barabara kujengwa upya

0
40


By Haika Kimaro, Mwananchi [email protected]

Mtwara. Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mtwara imeagiza baadhi ya barabara zilizo chini ya Wakala wa barabara Mijini na Vijijini (Tarura) manispaa ya Mtwara Mikindani na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kurudiwa kutokana na kujengwa chini ya kiwango.

Hatua hiyo imekuja baada ya mkuu wa Mkoa huo, Gelasius Byakanwa kuahidi kuunda kamati kufuatilia ujenzi wa barabara za Tarura, kubainika kuwepo kwa upungufu.

Upungufu huo ni kutolewa kwa  mikataba kwa makandarasi wenye uwezo mdogo au wenye gharama  ndogo isiyotekelezeka.

Akiwasilisha taarifa ya kamati aliyoiunda katika kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Mtwara leo Jumanne Julai 16, 2019, Byakanwa amesema kamati hiyo imetoa majibu inayoeleza baadhi ya halmashauri zimefanya vyema na nyingine kutofanya vizuri.

Amesema kamati ilibaini matatizo katika manunuzi na tayari wameshakutana na menejimenti ya Tarura katika halmashauri na Mikoa kuwekeana utaratibu na mwisho.

“Matatizo makubwa ya Tarura yapo Mtwara Mikindani lakini na halmashauri ya Masasi na baadhi ya barabara tumeagiza warudie kujenga. Kilichojitokeza kwa Tarura ni kutoa kandarasi au kutoa mikataba kwa makandarasi wenye uwezo mdogo ambapo hawawezi kutekeleza miradi inayotekelezwa na Tarura,” amesema Byakanwa

Amesema amewaagiza mameneja wote wa Tarura Mtwara kumpelekea orodha ya makandarasi na kufanya uchaguzi kulingana na uwezo wao.

 

Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here