R. Kelly ageuka dhahabu nchini Ujerumani, Mapromota walazimika kubadilisha ukumbi

0
58


Licha ya kuandamwa na tuhuma za unyanyasaji kingono wanawake nchini Marekani, Msanii nguli wa muziki wa R’n’B nchini humo, R. Kelly ameendelea kuwavutia mashabiki wake duniani kote ikiwemo nchini Ujerumani.

R. Kelly

Kwa mujibu wa mtandao wa habari za burudani wa Veltra, umeripoti kuwa R. Kelly atatumbuiza mjini Ludwigsburg nchini Ujerumani mwezi April 12, 2019. Hii ni baada ya kubadilisha ukumbi mara mbili kutokana na uhitaji wa tiketi kuongezeka.

Awali R. Kelly alipangiwa kutumbuiza katika ukumbi wa MHP Arena unaochukua watu 7,200, uliopo mjini humo lakini baadae mapromota wakabadilisha ukumbi wa show hiyo na sasa itafanyika katika ukumbi wa
Ratiopharm Arena unaochukua watu 9,000 .

Image result for ratiopharm arena
Ratiopharm Arena
Image result for mhp arena
MHP Arena

Mtandao huo umeripoti kuwa, tayari tiketi zote 9,000 zimeshanunuliwa tangu watangaze show hiyo mwezi uliopita.

Hata hivyo, waandaaji wa show hiyo wamesema kuwa tarehe ya show inaweza ikasogezwa au watu kurudishiwa hela zao endapo R. Kelly atakutwa na hatia ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake.

Kwa sasa R. Kelly yupo chini ya uchunguzi na mamlaka za usalama za mjini Fulton, Georgia nchini Marekani, kuhusu tuhuma za unyanyasaji wanawake kingono.

Tayari Makampuni na wasanii waliowahi kufanya kazi na R. Kelly nchini Marekani, wamefuta nyimbo mitandaoni. Hii ni kutokana na tuhuma hizo zinazomkumba msanii huyo nguli wa muziki wa R’n’B duniani.Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here