Polisi wamethibitisha kuwa mwili ulioopolewa kutoka kwenye mabaki ya ndege, iliyoanguka umegundulika kuwa ni wa Emilliano Sala

0
56


Mwili ulioopolewa kutoka kwenye mabaki ya ndege iliyoanguka ni wa mchezaji soka wa timu ya Cardiff City, Emiliano Sala Polisi ya Dorset imesema. Sala, mwenye umri wa miaka 28, alikuwa akisafiri kwenda Cardiff ikatika ndege ambayo rubani wake alikuwa ni David Ibbotson, iliyopotea mnamo Januri 12.

Kwa mujibu wa BBC. Mwili wake ulipatikana Jumatano baada ya kugunduliwa kwa mabaki ya ndege hiyo Jumapili asubuhi.Polisi ya Dorset imethibitisha utambulisho wake Alhamisi usiku.

Katika taarifa yake, kikosi hicho kimesema: “mwili ulioletwa katika bandari ya leo Alhamisi Februari 7 2019, umetambuliwa rasmi kuwa wa mchezaji soka Emiliano Sala.

“Familia ya Sala na rubani David Ibbotson wamearifiwa kuhusu taarifa hii na wataendelea kupewa usaidizi na maafisa wa kitengo maalum.”

Kikosi cha uchunguzi wa ajali ya ndege awali kilieleza kwamba wakandarasi maalum wamejiunga katika operesheni hiyo, katika ‘hali yenye changamoto nyingi’.

Imefanyika ‘kwa heshima kubwa iwezekanavyo’ na familia za wote wawili ziliarifiwa kadri shughuli zilivyokuwa zikiendelea.

Mabaki ya ndege hiyo, iliyopotea wiki mbili zilizopita, yalipatikana kutoka huko Guernsey.

Ndege hiyo chapa Piper Malibu N264DB ilikuwa ikielekea kutoka Ufaransa kwenda Cardiff, baada ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Argentina kurudi kwa safari ya haraka katika klabu yake ya zamani Nantes siku mbili baada ya kutangazwa kuidhinishwa kwa mkataba wake wa thamani ya £15m kwenda Cardiff .

Ibbotson, mwenye umri wa miaka 59, kutoka Crowle, Lincolnshire kaskazini, alikuwa kwenye mawasiliano na waongoza ndege ardhini ndege hiyo ilipokatiza mawasiliano na kupotea kwenye rada mnamo Januari 21.

Shughuli rasmi ya kuisaka ndege hiyo ilisitishwa Januari 24 baada ya mamlaka kudai uwezekano wa kupatikana hai wawili hao ulikuwa “mdogo mno”.

Hata hivyo, mabaki ya ndege hiyo yalipatikana chini ya bahari baada ya wasamaria wema kuchangisha fedha zilizowezesha operesheni ya binafsi iliyoongozwa na mwanasayansi ya bahari David Mearns.

Juhudi za kuinyanyua ndege hiyo toka chini ya bahari zimeshindikana kwa sasa kutokana na hali mbaya ya hewa.

By Ally Juma.Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here