Newcastle yavunja rekodi ya uhamisho kwa kumsajili Miguel Almiron kutoka Atlanta

0
60


Haki miliki ya picha
Reuters

Newcastle imevunja rekodi yake ya miaka 14 ya uhamisho kwa kumsajili mchezaji raia wa Paraguay Miguel Almiron kutoka Atlanta United.

Haya ni makubaliano makubwa waliowahi kuyafikia kufikia sasa.

Miguel Almiron anajiunga na Newcastle kwa mkataba wa miaka mitano na nusu.

“Nina furaha sana na hamu kubwa kuanza kucheza na kukutana na wachezaji wenzangu,” anasema Miguel.

  • Je, unawajua wachezaji ghali zaidi kuwahi kuuzwa mwezi Januari?
  • Fellaini akubali kuhamia ligi ya China

“Ligi ina ushindani mkubwa, hii ni klabu ya kihistoria, na Rafa Benitez mwenyewe ndio sababu niko hapa leo.

“Nadhani ni jukumu kubwa, jambo linalopendeza, na nitajaribu kufanya kila niwezalo kulipa imani ambayo klabu inayo kwangu.”

Haki miliki ya picha
Getty Images

Miguel Almiron ni nani?

Almiron amechangia ushindi mara 13 kwa Paraguay na amefunga magoli 13 msimu uliopita wakati Atlanta iliposhinda taji la MLS kwa mara ya kwanza.

Mshambuliaji huyo amefunga magoli 21 katika mechi 62 za ligi alizocheza, akiwa amewahi kuichezea Cerro Porteno nyumbani na timu ya Argentina Lanus.

Aliwahi pia kuwa bingwa wa ligi ya Argentina mnamo 2016 baada ya kuicheza Lanus mechi 12 katika divisheni ya Primera.

  • Boateng ajiunga na Barcelona
  • Chelsea yamnasa Gonzalo Higuain

Uhamisho wa Miguel Almiron kuingia Newcastle unamfanya kuwa mchezaji ghali zaidi kuuzwa kutoka ligi kuu ya soka Marekani.

“Tulikuwa tunamfukuzia Miguel Almiron kwa muda,” amesema meneja wa Newcastle Rafael Benitez. ” Tuliona mchezaji aliye na kasi katika ushambuliaji, anayeweza kucheza nyuma ya mshambuliaji.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Newcastle imevunja rekodi ya uhamisho ya thamani ya pauni milioni 16 zilizolipwa kwa Real madrid kumsajili Micheal Owen mnamo 2005

  • Pep Guardiola amnyima Kompany mkataba mpya

“Nina furaha kwamba jitihada kubwa za chini kwa chini zimemalizika vizuri na namshukuru kila mtu kwa usaidizi wake.”

Haki miliki ya picha
Getty Images

Miguel Almiron ni mchezaji wa pili kusajili na Newcastle leo. Beki kushoto Antonio Barreca alisajiliwa leo asubuhi.Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here