Mwana FA uso kwa uso na Jose Mourinho, afunguka alichomuambia ‘Maneno mabaya yote nimeyaficha’

0
27


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Mwana FA hapo jana alikuwa jijini Manchester nchini Uingereza kuishuhudia timu yake ya Manchester United wakati ilipowakabili wagonga nyundo West Hama United.

Kwenye mechi hiyo United iliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 1 yakifungwa na kiungo Paul Pogba.

Mbali na kushuhudia mashetani hao wekundu, Mwana FA alipata bahati ya kukutana na kupiga picha na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mreno Jose Mourinho.

Katika picha aliyoweka kwenye mtandao wake wa kijamii FA amendika kuwa amefurahi kukutana na kocha huyo na kumtakia bahati njema popote atakapojaaliwa kupata klabu ya kuifundisha.

”Mara paaap,chuma hiki hapa..nikifute kazi tena?😂..no man natania ,nilifurahi kukutana na Jose Mourinho leo..yale maneno mabaya yote nikayaficha,nikamshukuru kwa nyakati nzuri alipokuwa kwetu na kumtakia bahati njema popote anapokwenda..na kuwa mimi ni mshabiki wake mkubwa,hasa anapoanza kuchonga..i feel good kukutana na this great man!Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here