Mrundikano wa vitu watoa ishara ya vile sayari zinavyoundwa

0
83


Haki miliki ya picha
NASA

Image caption

Mchoro wa sayari iliojaa miamba

Wataalam wa angani wanasema kuwa wana ushahidi wa kugongana ana kwa ana kwa sayari mbili zilizoko katika mfumo wa nyota ulio mbali.

Wanaamini vitu wiwili viligongana ili kutoa dunia iliojaa vyuma , ambayo ina ukubwa mara 10 ya dunia ya kawaida.

Mgongano kama huo huenda ndio uliosababisha kuundwa kwa mwezi yapata miaka bilioni 4.5 iliopita.

Uvumbuzi huo ulifanywa na wataalam kutoka kisiwa cha Canary waliokuwa wakichunguza mfumo wa nyota yapata miaka 1,600 iliopita.

Sayari moja kwa jina Kepler inadhaniwa kumiliki vyuma ambavyo ni asilimia 70 ya uzito wake huku uzito uliosalia ukiwa na miamba.

Sayari nyengine karibu na nyota kwa jina kepler ni mara 1.5 kwa ukubwa ikilinganishwa na dunia lakini ni nyepesi.

Mfumo uliojawa na vurugu

Wanasayansi wanaamini sayari hiyo iliojaa vyuma iliundwa wakati ilipogongana na kitu chengine kwa kasi ya juu na kuangusha vitu vilivyokuwa juu yake .

Walichanganua kwamba sayari hizo zilizogongana huenda zilikuwa zikisafiri kwa kilomita 60 kwa sekunde .

Mwanzilishi mwenza Dkt. Zoe Leinhardt kutoka Chuo kikuu cha Bristol amesema kuwa kundi lao lilitumia aina tofauti ya kompyuta ili kujaribu mawazo hayo.

Wazo jingine ni kwamba kepler iligongwa mara kadhaa na vitu vidogo vidogo .

Tatizo la uchunguzi huo ni kwamba ni kwa nini haswa kitendo hicho kilitokea katika kepler 107c?.

”Inaonekana kuwa rahisi kwa mimi kuelewa na kufanya kupitia kisa kimoja lakini haimanishi kwamba kulikua na mgongano mmoja pekee”.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Uchunguzi huo ulifanyika katika eneo la Telescopio Nazionale Galileo huko La Palma

Mwanzilishi mwenza Dkt. Chris Watson wa chuo kikuu cha Queen mjini Belfast, alisema kuwa mfumo huu huenda ukawa eneo lililojaa mgogoro.

”Sasa ndio tunaona mabaki ya migongano ya kasi kati ya vitu viwili”, alisema.

”Tumepata sayari mbili katika mzunguko mmoja karibu na nyota ile ile lakini zikiwa na uzito tofauti”, aliambia BBC News.

Sayari moja ina miamba mingi huku nyengine ikiwa imetengezwa kutokana na vitu vizito zaidi kama vile chuma.

Njia ya pekee inayoweza kuelezea haya yote ni kwamba mojawapo ilikuwa na sakafu iliojaa miamba ambayo ilivunjika baada ya mgongano.

Wazo jingine ni kwamba mionzi kutoka kwa nyota ilitoa gesi kutoka kwa kile ambacho kingetajwa kuwa sayari ndogo ndogo.

Mpango huu ungesababisha sayari ya Kepler 107b kuwa nzito zaidi ya 107c.

Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Nature Astronomy , unazua maswali mapya kuhusu mifumo inayoumbwa na kuishi eneo mbali na duniani.Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here