Mbele ya Rais Magufuli, CCM yafanya uteuzi wa mgombea ubunge jimbo la Arumeru

0
34


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, imemteua Dkt. John Danielson Pallangyo kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki.

Awali Tume ya Uchaguzi ilitangaza uchaguzi mdogo wa marudio kuwa utafanyika mwezi Mei 19, 2019.

Jimbo la Arumeru Mashariki lilikuwa wazi baada ya aliekuwa Mbunge wake, Joshua Nassari kuvuliwa ubunge na Spika kutokana na kutohudhuria vikao vitatu.

Chama cha Mapinduzi kimefanya Kikao cha Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) leo mchana jijini Dodoma wakiogozwa na Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho.

indexSource link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here