Marekani: Kiongozi wa ujasusi aamua kujiuzulu, Korea kaskazini, Urusi na Iran zausishwa 

0
30


Mkurugenzi wa idara ya ujasusi Marekani, Dan Coats ni kiongozi wa hivi karibuni kujiuzulu katika utawala wa Trump.

Image result for Dan Coats

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Rais Donald Trump alituma ujumbe kwenye twitter akisema Coats atajiuzulu Agosti na kwamba atamteua mbunge wa Texas John Ratcliffe kuichukua nafasi hiyo.

Amesema kuwa Ratcliffe ataongoza “na kuhimiza ukubwa wa taifa” analolipenda.

Coats na Trump wametofuatiana mara kwa mara kuhusu Urusi na Korea kaskazini. Kama mkurugenzi wa idara ya kitaifa ya ujasusi, lilikuwa ni jukumu la Coats kushughulikia mashirika 17 ya ujasusi nchini likiwemo la CIA na NSA.

Lakini katika kipindi kizima cha uhudumu wa Coats, mitazamo yake yalipingwa mara kwa mara na rais, ambaye amekuwa akiyashutumu mashirika ya ujasusi.

Mnamo Januari rais aliwashutumu wakuu wa ujasusi kwa kuchukulia kwa urahisi tishio la Iran pasi kuchukua hatua.

Coats ni afisa wa hivi karibuni katika msururu wa maafisa chini ya utawala wa Trump kuondoka White House, aliyekuwa waziri wa ulinzi James Mattis na waziri wa mambo ya kigeni Rex Tillerson ni miongoni mwao.

Kwanini Coats ameondoka?

Katika barua yake ya kujiuzulu kwa rais, bwana Coats amesema jamii ya majasusi Marekani imekuwa na “nguvu zaidi ya ilivyoshuhudiwa” wakati wa muda wake wa miaka miwili na nusu ya kuhudumu.

“Kutokana na hilo, ninaamini muda umewadia kwangu mimi kusogea katika ukurasa mwingine wa maisha yangu,” aliandika.

Coats amesema mnamo Februari kuwa rais alimuomba asalie katika wadhifa huo, hatahivyo tofauti zao kuhusu sera za kigeni zilionekana kutopatana mara nyingine.

Dan Coats testifies to the Senate Intelligence Committee hearing

Inaarifiwa Dan Coats alitofautiana mara kadhaa na Donald Trump kuhusu Iran, Korea kaskazini na Urusi

Zaidi walitofuatiana kuhusu Urusi kuingilia kati uchaguzi Marekani, mkataba wa nyuklia wa Iran na jitihada za Trump katika kuidhinisha mtazamo mpya na Korea kaskazini.

Likimnukuu afisa wa zamani wa ujasusi, gazeti la The Washington Post limeripoti kuwa Coats alitambua kwamba hangekuwa na budi ila kuondoka katika wadhifa wake kutokana na uhusiano wake wenye utata na Trump.

Coats, afisa huyo wa zamani ameliambia gazeti hilo kuwa alihisi kutengwa na rais kuhusu masuala ya usalama wa kitaifa.

Mwaka jana, mkuu huyo wa ujasusi alikiri kuwa Trump hakumuarifu kuhusu mkutaon wake wa faragha na rais wa Urusi Vladimir Putin huko Helsinki.

“Angeniuliza kuhusu namna mkutano huo ulivyopaswa kufanyika, Ningependekeza njia nyingine,” Coats amesema kuhusu mkutano huo.

Alicheka kwa mshangao aliposikia kuhusu ziara iliyopendekezwa ya rais Putin katika ikulu ya Marekani White House, na kuuambia umati katika hafla moja kuwa : “Hiyo itakuwa ziara maalum.”

Dan Coats ni nani?

Mwanadiplomasia wa zamani, Coats amehudumu kama mkurugenzi wa idara ya taifa ya ujasusi tangu Machi 2017, alipomrithi James Clapper.

Alizaliwa Jackson, Michigan, Coats alihitimu katika vyuo vikuu viwili kwa shahada ya sayansi ya siasa na sheria katika miaka ya 60.

Alihudumu kwa mihula miwili kama seneta wa Indiana, kuanzia 1989 hadi 1999 na kwa mara nyingine kuanzia 2011 hadi 2017.

Coats pia alihudumu kama balozi wa Marekani kwa Ujerumani kuanzia 2001 hadi 2005 katikati ya muhula wake katika seneti.

Mrithi wake ni nani?

Mfuasi maarufu wa rais na sera zake, Ratcliffe amehudumu kama mbunge wa Texas 4th District tangu 2015.

Trump amesema Ratcliffe ni “mbunge anayeheshimika pakubwa” ambaye “ataongozana kuhimiza ukubwa wa taifa analolipenda”.

John Ratcliffe questions former special counsel Robert Mueller in Congress

John Ratcliffe anatarajiwa kuteuliwa kuichukua nafasi ya Dan Coats kama mkurugenzi wa idara ya taifa ya ujasusi

Ilimradi uteuzi wake utaidhinishwa, mtazamo wa Ratcliffe unatarajiwa kuwiana na wa Trump zaidi katika wadhifa wake mpya.

Wiki iliyopita, Ratcliffe alimteta rais wakati wa kutoa ushahidi wa Robert Mueller, aliyeongoza uchunguzi wa miaka miwili kuhusu Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani mnamo 2016.

Ratcliffe alisema Mueller hana mamlaka “ya kubaini iwapo Trump ana hatia au kumuondoshea makosa”.

Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here