Kampuni yatozwa Tsh. Bilioni 4 kwa kosa la kum-tag na kutumia vibaya jina la Kim Kardashian kwenye mtandao wa Instagram, Watumiaji wengine wapigwa onyo

0
31


Hakuna ubishi kwa sasa mtandao wa Instagram umekuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa wasanii na watu wengine maarufu na ndio mtandao pekee wenye watumiaji hai (active users) wengi kwa hapa Tanzania.

Ukweli ni kwamba mastaa wengi duniani kwa sasa wanaingioza pesa nyingi sana kupitia matangazo wanayoposti kwenye kurasa zao za Instagram.

Na ukweli ni kwamba hata Makampuni makubwa yamekuwa yakiwatumia wasanii hao kutangaza bidhaa zao na yamekuwa yakiingiza faida kubwa kupitia matangazo hayo, Jambo ambalo linapelekea kwa sasa mtandao wa Instagram kuwa chanzo cha mapato kwa watu maarufu na hata wale wenye ‘page’ zenye wafuasi wengi.

Sasa kufuatia ukweli huo, Kampuni moja ya mambo ya fasheni nchini Marekani iitwayo, Missguided imepigwa faini ya dola milioni $2.8 sawa na Tsh bilioni 4.2 kwa kosa la kumtag mwanamitindo Kim Kardashian na kutumia brand yake kibiashara.

Kampuni hiyo inayotumia jina la @missguided imekuwa ikim-tag Kim na kisha kueleza kuwa nguo hizo alizovaa zipo kwenye maduka yao, jambo ambalo limeongeza mauzo ya nguo kutoka kwenye maduka yao.

Kim ameshinda kesi hiyo wiki iliyopita, Baada ya mwanasheria wake kupeleka shauri hilo la madai mahakamani kwa kutumia kibiashara brand ya jina la Kim Kardashian kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha, Mahakama mjini California ambayo ndiyo iliyotoa hukumu hiyo, Imeitaka kampuni ya Missguided kuacha kutumia kabisa picha za Kim na kuitaka pia ifute picha zote za mrembo huyo kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii na website.

Tayari kampuni hiyo imetii agizo hilo na imefuta picha zote za Kim Kardashian walizowahi kupost kwenye ukurasa wao wa Instagram.

Kwa upande mwingine, Mwanasheria wa Kim ameyaonya makampuni mengine yanayotumia brand ya mteja wake kibiashara kuacha mara moja mchezo huo.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2018, Kim Kardashian alishika nafasi ya 4 akiwa nyuma ya Kylie Jenner, Selena Gomez na Cristiano Ronaldo.

Kim Kardashian anatoza Euro 547,000 sawa na Tsh bilioni 1.6 kwa kila post moja ya Tangazo.

 Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here