Hivi ndivyo Guardiola alivyo bashiri bingwa wa Premier League atakavyopatikana msimu huu

0
104


Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa kutokana na ushindani mkubwa uliyopo kwa sasa katika mbio za kuwania ubingwa wa Premier League hivyo inaonyesha wazi mshindi wa taji hilo atapatikana kutokana na tofauti ya mabao.

Guardiola akiiyongoza Manchester City inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa nyuma kwa tofauti ya pointi tatu dhidi ya Liverpool na huwenda zikawa sawa kama watashinda mchezo wao wa Jumatano dhidi ya Everton.

Mabingwa hao watetezi walirudi kwenye mbio za kuwania taji hilo baada ya Liverpool kutoka sare kwenye mechi zake mbili za hivi karibuni huku, Guardiola akiamini timu ya mshindani wake, Jurgen Klopp italazimisha kupata matokeo kwenye kila mchezo.

“Jambo la kwanza ni kushinda mechi, kama unapata nafasi ya kufunga magoli ni bora kufunga haswa na kama unaweza kuepuka kufungwa fanya hivyo kwa sababu huwenda bingwa wa Premier League akapatikana kwa tofauti ya magoli,” amesema Guardiola.

“Siendi kuwaambia vijana wangu wafunge mabao 25 – 0 hapana, kwanza nawaambia wahakikishe tunashinda mechi alafu jambo la pili ni kufunga magoli kwa sababu huwenda ikatokea bingwa akapatiana kwa tofauti hiyo ya magoli,”

“Ninahakika bingwa safari hii ataamuliwa kwenye mchezo wa mwisho wa ligi ama miwili ya mwisho.”Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here