Hasara baada ya moto kuteketeza eneo la mlima Kenya

0
22


Image caption

”Wanyama wadogo waliteketea huku wakubwa wakihama mbuga ya mlima Kenya” anasema Mercy Juma- mwandishi wa BBC aliyetembelea eneo la mlima Kenya

Kwa zaidi ya wiki mbili wazima moto walijitahidi kuzima moto mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika mlima Kenya, ambao ni mlima wa pili kwa urefu barani Afrika na yenye minara mirefu ya maji,

Mwandishi wa BBC Mercy Juma alikwenda kutathmini hasara .zilizosababishwa na moto huo anasema, maelfu ya hekari ya sehemu hio muhimu ya mlima yameharibika

”Wanyama wadogo waliteketea huku wakubwa wakihama mbuga hio” amesema Mercy ambaye amekuwa kwenye eneo hilo la mlima Kenya na kuongeza kuwa:

”Katika kipindi cha saa mbili za kwanza tulipokua tukipanda mlima kenya, huku tukipitia katika msitu wa Mianzi na kushuhudia kupotea kwa upeo wa mawingu”

Image caption

Moto uliowaka katika maeneo tofauti ya msitu uliteketeza sehemu kubwa ya mbuga ya taifa katika mlima huu kwa wiki tatu zilizopita.

Eneo la mlima Kenya lina harufu ya nyasi zilizoungua, kuna masizi kila mahali na mashina ya miti iliyongua na hili linaonekana katika sehemu kubwa sana.

  • Tundu Lissu kufungua shauri kudai stahiki zake

Maafisa wa misitu wameiambia BBC kuwa kwamba wiki mbili zilizopita sehemu hiyo ilikua ni ya kupendeza sana, lakini sasa ni sehemu ambayo haina mvuto wowote , imeungua kupita kiasi.

Moto uliowaka katika maeneo tofauti ya msitu uliteketeza sehemu kubwa ya mbuga ya taifa katika mlima huu kwa wiki tatu zilizopita.

Image caption

Moto huo ulianzia ndani ya msitu wa mianzi katika mlima Kenya

Mkuu wa huduma za dharura katika mbuga ya wanyama ya mlima kenya George Ombuki anasema,

Eneo kubwa lililoungua lilikuwa na misitu likiwa ni karibu hekari 80 na bado baadhi ya sehemu kwa sasa kuna moto ambao unaendelea kuwaka.

Moto huo ulianzia ndani ya msitu wa mianzi, jambo ambalo linaleta ni chamgamoto kubwa kutokana na ugumu wa kudhibiti moto katika msitu wa mianzi.

Image caption

Doreen Kagendo mkulima wa mashamba ya mboga katika eneo la mlima Kenya

Msitu huoni tegemeo kubwa la uchumi wa Kenya na kivutio muhimu cha utalii ambacho ukifahamika kwa kuwa na aina mbali mbali ya wanyama pori.

Lakini pia msitu wa mlima Kenya ni chanzo muhimu cha upatikanaji wa maji na sehemu muhimu ya uzalishaji wa nishati ya umeme nchini Kenya.

Kuna mshamba mengi katika maeneo yanzayozunguka mlima huu ,na ukiwa kwenye mashamba haya unaweza kupata picha nzuri ya theluji kwa uzuri zaidi.

Doreen Kagendo mama wa watoto 6 anayemiliki moja ya mashamba ya mboga katika eneo la Sirimon, anasema wanategemea kilimo eneo hilo.

Image caption

George Ombuki afisa wa idara ya wanyamapori nchini Kenya anasema moto wa hivi karibuni ulisababishwa na binamu

Eneo la mlima Kenya moja ya maeneo yanayostawisha kwa wingi mazao ya chakula kwa wingi nchini Kenya.

Lakini kutokana na uharibifu wa msitu na mashamba, wanamazingira wana hofu kwamba, hili linaweza kuleta mdhara makubwa

Wakati inaaminiwa kuwa ni jambo la kawaida kwa moto kuwaka kwenye misitu na nyikani, George Ombuki afisa wa idara ya wanyamapori nchini Kenya anasema moto wa hivi karibuni ulisababishwa na binamu.

Picha: Peter NjorogeSource link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here