George Jonas: Muhandisi maarufu wa Tanzania anayefanya kazi na kampuni ya Boeing ashinda tuzo Marekani

0
69


Haki miliki ya picha
George Jonas/Twitter

Image caption

George Jonas: Muhandisi maarufu wa Tanzania anayefanya kazi na kampuni ya Boeing ashinda tuzo Marekani

George Jonas, raia wa Tanzania anayefanya kazi na kampuni ya Boeing nchini Marekani amepata tuzo ya muhandisi mweusi Mwafrika bora wa mwaka {Beya}wikendi iliopita.

Alishinda tuzo ya Walt W Braithwaite Legacy Award wakati wa kongamano hilo.

Bwana Jonas kwa sasa anafanya kazi na kampuni ya Boeing kama muhandisi wa usalama katika ndege ya 777X.

Beya ni mojawapo ya tuzo kuu nchini Marekani zinazopewa maafisa waliobobea katika nyanja za sayansi, teknolojia, Uhandisi na hesabati.

Ni miongoni mwa watu 41 duniani waliopokea tuzo za Beya katika orodha tofauti.

Anajumuika na wengine kutoka kampuni ya Boeing akiwemo Bwana Raenaurd Turpin, muhandisi mkuu wa kampuni hiyo aliyepokea tuzo ya mchango wa kiufundi katika viwanda na bi Tiera Fletcher, ambaye ni muhandisi wa uzinduzi wa mifumo na mitindo ya angani, ambaye alipokea tuzo ya muhandisi bora anayechipuka.

Wafanyikazi wengine wa kampuni hiyo ambao watazawadiwa ni mkurugenzi wa maswala ya ajira na wafanyakazi katika Boeing Kusini mwa mji wa Carolina Akeem Iman Jones kwa tuzo ya Dave Barclay Affirmative Action Award na Leo Brooks Jr, makamu wa rais wa Boeing , Ulinzi, Angani, Usalama na operesheni za serikali ambaye alipokea tuzo ya ufanisi mkubwa viwandani.

Bwana Jonas alipata umaarufu nchini Tanzania wakati kampuni ya Air Tanzania ATCL ilipopokea ndege ya kwanza aina ya Boeing 787-800 Dreamliner ,mnamo mwezi Julai mwaka uliopita.

Bwana Jonas , mwenye umri wa miaka 41, anayetoka katika jimbo la Mbeya , ni mmojwapo wa mafundi wa kampuni ya Boeing walioshiriki katika kuunda ndege hiyo yenye viti 262.

Bwana Jones alijiunga na Boeing mwaka 2011.

Kabla ya kujiunga na Boeing, alikuwa mfanyikazi wa Bombardier, ambapo alitambuliwa kwa mchango wake mkubwa katika mabadiliko ya mradi wa Bombardier Learjet mwaka 2009.

Masomo yake

Masomo hayo yalitarajiwa kumpeleka katika kampuni ya Bombardier, kampuni ya uchukuzi wa ndege ya Canada ilioko katika mji wa Montreal, Quebec.

Akiwa nchini Marekani, alituma maombi ya kutaka kusoma katika chuo kikuu na akafanikiwa kusajiliwa na chuo kikuu cha Wichita ambapo alisomea shahada ya uhandisi wa mitambo ya kielektroniki pamoja na hesabati.

Alifanya mafunzo yake katika tawi la Bombaridier lililopo Wichita 2005, huku akihusika na utengezaji wa ndege za watu binafsi pamoja na zile za kijeshi.

Alifanya kazi katika kampuni hiyo kwa miaka minne kabla ya kujiunga na Boeing 2011 kama muhandisi wa kielektroniki wa mitambo ya ndege za kibiashara.

Alihusika na mifumo yote ya kuendesha ndege hiyo.

Wakati mmoja alipokuwa katika mtandao akapata tangazo la Boeing na kuamua kujaribu kutuma ombi.

”Siku moja nilipokuwa kazini nilipokea simu kutoka Boeing, ikinielezea kwamba nilikuwa miongoni mwa watu 50 walioorodheshwa katika mahojiano ya kazi. Walinitumia nauli ya ndege. Nilienda katika Muhandisi maarufu wa Tanzania ashinda tuzo Marekanimahojiano hayo, nikiwa sina wasiwasi, kwasababu tayari nilikuwa nimeajiriwa na Bombadier”, alisema.

Baadaye alipatiwa habari njema kwamba amepata kazi na kwamba alifaa kuhamia katika jimbo la Seattle kufanya kazi na Boeing.

Akiwa huko alijifunza mambo mengi .

Mwaka 2015, alisomea shahada ya uzamili katika uhandisi wa mitambo katika chuo kikuu cha Washington. Mbali na mafunzo hayo pia alijifunza kuhusu usalama wa ndege . Pia anamiliki cheti cha usimamizi wa miradi kutoka chuo kikuu cha Stanford, alisema.

Nchini Tanzania , ameanzisha mradi kwa jina STEM.

Maana ya STEM ni Sayansi, Teknolojia, Uhandisi{Engineering} na Hesabati{ Mathematics} kwa lengo la kuimarisha mafunzo kwa msingi wa mradi huo na kujumuisha mafunzo hayo katika mtaala wa sayansi na hesabati.

Boeing 787-8 Dreamliner ni ndege ya aina gani?

Ndege hiyo ya Tanzania ilisafiri kutoka uwanja wa Paine mjini Seattle, Washington safari ya umbali wa saa 22.

Boeing 787-8 Dreamliner ni ndege ya kisasa ambayo hutumia injini ya kisasa zaidi aina ya Trent 1000 TEN. Bei yake inakadiriwa kuwa $224.6 milioni.

Injini hiyo inatumiwa katika ndege zote mpya aina ya Boeing 787 na huhifadhi mafuta, ambapo huwa inachoma mafuta kwa kiwango cha asilimia tatu chini ukilinganisha na ndege za aina hiyo na kuyatumia vyema zaidi.

Hilo huiwezesha kupunguza matumizi ya mafuta ukilinganisha na ndege nyingine za ukubwa kama wake kwa asilimia 20-25, aidha hupunguza utoaji wa gesi chafu kwa kiwango sawa na hicho.

Aidha, huwa haipigi kelele sana. Ni ndege ambayo imechukua uwezo na kasi ya ndege kubwa aina ya ‘jet’ na kuuweka kwenye ndege ya ukubwa wa wastani.

Ina uwezo wa kubeba abiria 262 ni ya kisasa zaidi kuwahi kumilikiwa na serikali ya Tanzania. Mataifa mengine kama vile Kenya na Ethiopia hata hivyo yamenunua ndege kama hizo kadha.

Ndege hii ina uwezo wa kusafiri kiilomita 13,620 kwa wakati mmoja na urefu wake ni mita 57. Upana wa mabawa yake ni mita 60. Urefu wake kutoka chini hadi juu ni mita 17.

Rais Magufuli aligusia hilo aliposema: “Ndege hii ni ya kisasa na kote walikopita walikuwa wana uwezo wa kunipigia simu na kuongea nao angani.”

Ethiopia ilikuwa nchi ya kwanza duniani kando na Japan kuanza kutumia ndege aina ya Boeing 787-8 Agosti 2012.Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here