Fally Ipupa aendelea kuwaburuza wasanii wa muziki Afrika Mashariki na Kati kwenye mtandao wa YouTube

0
59


Msanii wa muziki kutoka DR Congo, Fally Ipupa ameendelea kuwaburuza wasanii wenzake wa muziki kutoka Afrika Mashariki na Kati kwa video zake kutuzamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube.

Fally Ipupa kwa sasa ndiye msanii pekee Afrika Mashariki na Kati, ambaye video zake za nyimbo mbili kwenye mtandao wa YouTube zimetazamwa mara milioni 50 (views 50M).

Wimbo wa Eloko Oyo wiki iliyopita umefikisha views milioni 50 ukiwa na miaka miwili tangu uwekwe kwenye mtandao huo.

Rekodi hiyo, ameivunja yeye mwenyewe baada ya wimbo wake wa Bad Boy akiwa na mrembo, Aya Nakamura kutoka Ufaransa .

Kwa upande mwingine, nyimbo ambazo zinafuatia kukaribia rekodi ya nyimbo hizo mbili ni wimbo wa Nana wa Diamond Platnumz aliomshirikisha Mr Flavour.Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here