Caf: Simba yailaza Al-Ahly na kujipatia pointi tatu kombe la Caf

0
67


Haki miliki ya picha
Tff

Image caption

Wachezaji wa Simba wakimenyana na wenzao wa Al-Ahly ya Misri

Timu ya Simba kutoka nchini Tanzania imejipatia ushindi 1-0 dhidi ya Al Ahly kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika Kundi D .

Bao la Simba lilifungwa na aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Gor mahia kutoka Kenya Meddie kagere kunako dakika ya 66.

Simba walijipatia bao hilo katika kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kuwa kigumu huku timu zote mbiuli zikijaribu kuingia katika lango la timu nyengine.

Simba hatahivyo ndio iliotawala kipindi cha kwanza huku ikishindwa kupata mabao ya mapema licha ya kupata nafasi tatu za wazi.

Katika mechi ya mkondo wa kwanza nchini Misri, Simba ambao walicharazwa mabao 5 bila jibu walionekana kuimarika tofauti na mechi hiyo ya Misri ambapo walifungwa mabao yote katika kipindi cha kwanza.

Nafasi za Simba

Nafasi ya kwanza ilikuwa dakika 9, Emmanuel Okwi aliwapiga chenga mabeki wa Al Ahly na kutekeleza shambulio ambalo lilinyakwa na kipa.

Maddie Kagere alipata pasi nzuri mbili dakika ya 12, ambapo alishindana na walinzi wa Al Ahly kabla ya nafasi na kupiga shuti lililopanguliwa na kipa na kuwa kona.

Kagere alipata fursa nyengine kunako dakika ya 40, baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Chama ambapo shambulizi lake lilipanguliwa na kipa na kusababisha kona.

Simba walifanya mabadiliko dakika 39, kwa kumtoa Asante Kwasi na kumuingiza nahodha msaidizi Mohamed ‘Tshabalala’.

Al Ahly walifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini muda mwingi walikuwa chini ya ulinzi wa Simba.

Baadaye nafasi ya John Bocco ilichukuliwa na Hassan Dilunga kipindi cha pili.

Iwapo Simba wangemakinika washambuliaji wao wote wawili Okwi na Kagere wangeweza kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa na magoli.Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here