Botswana yawapatia viongozi viti vilivyotengenezwa kwa kwato za ndovo

0
50


Image caption

Rais Mokgweetsi Masisi akikabidhi viti vilivyotengenezwa kwa kwato za ndovu kwa marais wenzake kutoka Zimbabwe, Zambia na Namibia

Viti vidogo vilivyotengenezwa kwa kwato za tembo vimewasilishwa kwa viongozi watatu wa Afrika na rais wa Botswana wakati wa kikao kilichojadili hali ya baadae ya mamalia.

Rais Mokgweetsi Masisi aliwakabidhi zawzdi hizo zilizokuwa zimefunikwa na kitambaa cha blu kwa wenzake kutoka Namibia, Zambia na Zimbabwe.

Nchi hizo zilizo pamoja na Afrika Kusini ,zinatoa wito wa marufuku kwa mauzo ya pembe za ndovu iondolewe.

Wanadai pesa zitokanazo na biashara hiyo hutumiwa katika miradi ya uhifadhi wa wanyamapori.

Uwindaji wa tembo ni tatizo kubwa kote barani Afrika na badhi wanakadiria kuwa tembo 30,000 kuuawa kila mwaka. Inasemekana ni tembo 450,000 ndio waliobakia barani Afrika.

Image caption

Kiti kilichotengenezwa kwa kwato za ndovu (kilichofunikwa kwa kitambaa cha blu) ambacho kilitolewa kama zawadi kwa rais

Kampeni za kimataifa za kupiga marufuku mauzo yote ya pembe za ndovu kama njia ya kuzuwia uwindaji haramu zimekuwa zikiongezeka, lakini lakini kumekuwa na kutokubaliana juu ya namna ya kudhibiti tembo wanaovuka mipaka nakuingia kwenye makazi ya watu.

Mwenyeji wa mkutano Botswana, ambayo ilikuwaina wanyama hao 130,00, inakabiliwa na mzozo baina ya binadamu na ndovu.

Zawadi ya kushangaza ya viti vilivyotengenezwa kwa kwato ilituma ujumbe mkubwa wa kuunga mkono kampeni hiyo, alisema mwandishi BBC Alastair Leithead.

Haki miliki ya picha
AFP

Rais Masisi, ambaye aliingia madarakani mwaka janaamebadilisha sera uhifadhi wa ndovu iliyoanzishwa na mtangulizi wake, Ian Khama.

Ingawa ni marufuku kuchinjwa kwa ndovu nchini Botswana kuna uungaji mkono mkubwa kutoka kwa jamii wa kuondolewa kwa marufuku ya uwindaji wa wanyama hao, jambo ambalo huwa ni ajenda muhimu katika mwaka wa uchaguzi.

Image caption

Namibia, Afrika Kusini na Zimbabwe huruhusu uwindaji wa ndovu

Wakosoaji hata hivyo wanasema itawazuwia watalii tajiri wanaochangia chanzo cha pili cha mapato ya taifa ya pesa za kigeni kwenda nchini humo.

  • Liverpool yafufuka na kuing’oa Barcelona klabu bingwa Ulaya

Namibia, Afrika Kusini na Zimbabwe huruhusu uwindaji na zinaunga mkono ombi la taasisi zinazosimamia biashara ya viumbe walio katika hatari ya kutoweka kuruhusu mauzo ya pembe za ndovu kwa ajili ya kufadhili uhifadhi wa wanyamapori.Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here