Boeing 737 Max: Rwanda yapiga marufuku hizo kuruka katika anga yake

0
24


Haki miliki ya picha
Stephen Brashear

Shirika la usafiri wa ndege Rwanda limetoa agizo kwa marubani na kampuni za ndege kutoendesha ndege za Boeing 737 Max 8 ana 9 katika anga ya Rwanda.

Rwanda sasa imejiunga na mataifa mengine duniani ambayo yamepiga marufuku usafiri wa ndege hizo za aina ya Boeing 787 Max 8 na Max 9.

Hii inafuata ajali ya ndege ya Ethiopia Airlines Jumapili ilioanguaka muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji mkuu Addis Ababa na kusababisha vifo vya watu 157.

Taarifa zinaeleza kwamba Rwanda ilikuwa na mipango ya kukodisha ndege mbili za aina hiyo Boeing 737- 800.

Hatahivyo, huenda mipango hiyo ikasitishwa kwa muda sasa wakati kukisubiriwa uchunguzi wa chanzo cha ajali ya ndege ya Ethiopia iliyoanguka Jumapili nje kidogo ya mji mkuu Addis Ababa.

Ndege kama hiyo ya kampuni ya Lion Air, ilianguka kutoka pwani ya Indonesia Oktoba mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 189.

Katika taarifa rasmi iliyowekwa kwenye mtandao wa twitter ya mkurugenzi mkuu katika shirika hilo la usafiri wa ndege Rwanda, Silas Udahemuka, RCAA limesema kwamba marufuku hiyo imeanza kufanya kazi mara moja.

“Shirika la usafiri wa ndege Rwanda kwa uwezo uliopewa katika kifungu cha 16 cha sheria za usafiri wa ndege nchini inaagiza marubani na kampuni za ndege zinazohudumu ndege za Boeing 737 – 8 Max na Boeing 737 – 9 Max, zisiendeshe usafiri wowote wa ndege hizo katika anga ya Rwanda mara moja,” inasema taarifa hiyo.

Marekani ni nchi ya hivi karibuni kusitisha usafiri wa ndege hiyo ya Boeing 737 Max yakiwemo mataifa mengine kama Uingereza, Umoja wa Ulaya, China India na Australia ambayo yote yameamua kusitisha usafiri wa ndege hizo.

Haki miliki ya picha
JONATHAN DRUION

Boeing 737 Max yasitisha matumizi ya ndege aina hiyohadiangalau Mei

Ndege zote za Boeing 737 Max 8 na 9 zimepigwa marufuku kuhudumu hadi angalau Mei baada ya ajali hiyo ya shirika la ndege la Ethiopia, Shirika la kitaifa la usafiri wa ndege nchini Marekani (FAA) limesema.

Ndege hizo hazitohudumu hadi mfumo wake wa uhudumu uimarishwe na uidhinishwe, FAA limesema.

Mkasa huo wa ndege nje kidogo ya mji mkuu Addis ulisababisha vifo vya watu 157 kutoka mataifa 35.

Ni ajali ya pili ya aina hiyo ya ndege ya 737 Max katika muda wa miezi mitano.

Baadhi ya watu wamegusia ufanano wa mikasa hiyo, huku baadhi ya wataalamu wakitaja data ya satelaiti na ushahidi kutoka eneo la mkasa kuonyesha uhusiano wa ajali ya ndege ya Ethiopia na ile ya iliyotokea Indonesia ya Lion Air mwaka jana.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Maafisa wanasema ni shughuli inayohitaji umakini mkubwa

Wachunguzi nchini Ufaransa wamepokea jukumu la kisanduku kinachonakili data ya safari hiyo ya ndege maarufu ‘black boxes’ wakijaribu kubaini chanzo cha ajali ya ndege hiyo ya Boeing 737 Max.

Huenda ikachukua muda kupata data ya awali, lakini mengi itategemea hali ya kisanduku hicho.Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here