Beki agoma kung'oka KMC

0
18


 

By ELIYA SOLOMON

BEKI  wa kati wa  KMC, Ally Ally anatarajia kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ambayo msimu ujao itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.
Ally ambaye kwa sasa amerejea kwao visiwani Zanzibar kwa mapumziko, alisema anajiona kuwa na furaha ndani ya KMC kwa hiyo hana mapango wa kutaka kuondoka.
Nyota huyo, alisema Yanga walimfuata wakitaka kumsajili  kipindi hiki cha usajili  lakini maamuzi yake ni kuendelea kuichezea KMC msimu ujao wa 2019/20.
“Yanga ni timu kubwa ambayo kila mchezaji anayechipukia anatamani kupata nafasi ya kuichezea, upande wangu ni tofauti napenda kucheza mpira sehemu ambayo najiona nina furaha nayo.
“Nimekuwa na msimu mzuri KMC kwa hiyo naona ni bora kuendelea kuichezea, kama kuondoka basi niende nje ya nchi ambako kuna ofa nimepata.
“Muda wangu wa mapumziko ukimaliza nitaenda kusaini mkataba mpya, kwa sasa nahitaji kutulia na familia yangu,” alisema beki huyo

Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here