Anthony Martial asaini kandarasi mpya itakayombakiza Man Utd mpaka 2024, Fellaini atua Shandong Luneng

0
67


Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Anthony Martial amefunga magoli 46 goals katika mechi 162 alizoichezea Manchester United

Mshambuliaji machachari wa Manchester United Anthony Martial amesaini kandarasi mpya na Manchester United itakayombakisha katika uga wa Old Trafford mpaka Juni 2024.

Martial mwenye miaka 23, alijiunga na United kutoka Monaco Septemba 2015 kwa pauni milioni 36, lakini hakuwa na furaha klabuni hapo mwaka 2018 na kocha aliyepita Jose Mourinho alikuwa radhi kumuuza.

Mkataba wake mpya utamfanya asalie na Mashetani Wekundu mpaka atakapotimu miaka 29, na kuna kipengele kinachoruhusu mkataba huo kuongezwa kwa mwaka mmoja.

  • Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 31.01.2019
  • Newcastle yavunja rekodi ya uhamisho

Kocha wa muda wa United Ole Gunnar Solskjaer amesema: “Kwa umri wake, ana ubongo mzuri wa mpira, ambao, ukijumuishwa na kipaji chake cha kipekee kinamfanya awe mchezaji mwenye mustakabali mzuri kabisa.”

Mwezi Juni, ajenti wa Martial alisema mteja wake alikuwa anataka kuhama, na Mourinho alikwa radhi, lakini uongozi wa United ulizima jaribio hilo na wakafungua ukurasa mpya wa majadiliano.

“Ningependa kumshukuru Ole na benchi lake la ufundi kwa kuniamini na kunifanya nikue mchezoni. Nafurahia wakati wangu klabuni. Toka siku nilipojiunga nimekuwa sehemu ya familia ya United na mapenzi ya mashabiki yamekuwa nguzo yangu,” amesema Matial.

Fellaini atua Shandong Luneng

Haki miliki ya picha
FELLAINI

Image caption

Fellaini (wapili kushosto) akiwa na jamaa zake kwenye uwanja wa ndege wakielekea Uchina

Manchester United wamefikia makubaliano na klabu ya Ligi ya Uchina Shandong Luneng juu ya uhamisho wa kiungo Marouane Fellaini.

Tayari kiungo huyo raia wa Ubelgiji amepita vipimo vya kiafya lakini hijawekwa wazi amehamia Uchina kwa kiasi gani.

  • Batshuayi atua Palace, Burnley yamsajili Crouch, Kagawa ajiunga na Besiktas

Fellaini, 31, alikuwa mchezaji mkubwa wa kwanza aliyesainiwa baada ya enzi ya Sir Alex Ferguson, akijiunga na Manchester Utd kwa kima cha pauni milioni 27.5 mwaka 2013 akitokea Everton.

Fellaini alitia saini kandarasi mpya ya miaka miwili Old Trafford mwezi Juni mwaka jana lakini hajawahi kukubalika na mashabiki wa United licha ya kukonga nyo za mameneja David Moyes, Louis van Gaal na Jose Mourinho.

Hata hivyo, Fellaini amecheza dakika tatu tu kwenye Ligi ya Premia katika mechi saba chini ya kocha wa muda Solskjaer.Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here