Ajali ya Morogoro: Majeruhi sita zaidi wafariki dunia

0
19


Ajali ya mlipuko wa lori la mafuta mjini Morogoro inaendelea kugharimu maisha ya watu na hivi sasa waliofariki kutokana na mkasa huo wa jumamosi asubuhi wamefikia 82.

Idadi hiyo imeongezeka baada ya majeruhi sita kati ya wale waliolazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuaga dunia, linaripoti gazeti la The Citizen.

Watu 62 walithibitishwa kufariki siku ya mkasa na zaidi ya 70 kujeruhiwa, na toka hapo idadi ya vifo imekuwa ikiongezeka taratibu.

Awali idadi ya majeruhi 46 walisafirishwa kutoka Morogoro mpaka Muhimbili kwa matibabu ya kibobezi.

Mpaka kufikia leo, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa Muhimbili, Bw Amini Algaesha idadi ya majeruhi waliosalia hospitalini hapo ni 32, kati yao 17 wapo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.

Huwezi kusikiliza tena

Kilichotokea Morogoro?

Wengi wa majeruhi waliokimbizwa Muhimbili walikuwa wameunguzwa na moto kwa asilimia 80 na kuendelea.

Mkasa huo ulitokea majira ya saa mbili asubuhi ya Jumamosi baada ya lori lilibeba shehena ya petroli kuanguka katika mji wa Morogoro, na watu kuanza kuchota mafuta yaliyomwagika kisha mlipuko mkubwa kutokea.

Kumekuwa na hisia tofauti juu ya ajali hiyo lakini Rais wa nchi hiyo John Magufuli amewataka wananchi wake kuacha kuhukumu waliofariki na majeruhi.

Huwezi kusikiliza tena

Miili ya waliofariki yawasili ili kuagwa shule ya pili ya Morogoro

”Naona watu wanasema kwamba hawa wote walienda kuiba , tusiwe majaji wengine walienda kusaidia huku wengine wakiwa wapita njia , Mwengine alikuwa safarini kuelekea Mtwara, akazuiliwa na moto ulipolipuka ukamkuta”, alisema Magufuli baada ya kuwajulia hali majeruhi siku ya Jumapili.

Baadhi ya waliofariki waliungua kiasi cha kutokutambulika na vipimo vya vinasaba vya jeni (DNA) kupitia ndugu waliopoteza wapendwa wao.

‘Tiba ya kisaikolojia’ yapelekwa Morogoro

Katika kukabiliana na athari ya janga hilo kwenye jamii, serikali ya Tanzania imetuma timu ya wataalamu wa ushauri, saikolojia na ustawi wa jamii mjini Morogoro kwenda kuwahudumia wale waliopoteza ndugu na jamaa ama kupata majeraha.

Kiongozi wa msafara huo wa wataalamu takribani 30, Dkt Naftali Ng’ondi kutoka Wizara ya Afya Tanzania ameiambia BBC kuwa timu yake ipo Morogoro tangu Jumatatu Agosti 12.

Huwezi kusikiliza tena

Mkasa wa Morogoro umewaacha wengi na msongo wa mawazo

“Yanapotokea matukio kama haya, wale ambao wamepatwa na majeraha pamoja na familia zilizoachwa na marehemu wanakuwa kwenye mshtuko pamoja na msongo wa mawazo kiasi cha kushindwa kurudi katika hali ya kawaida. Inapokuja tiba sasa tunasema ya nafsi na tiba ya roho, akili pamoja na utulivu wa kihisia kwa binadamu hilo linakuwa ni jukumu la wataalamu wanaohusika na huduma za kisaikolojia na kijamii,” ameeleza Dkt Ng’ondi.

Huduma ya wataalamu hao inafanyika hospitalini na majumbani ili kuchambua mahitaji yao na kisha kutoa ushauri, hususani wa kuondoa huzuni.

“Kikubwa tulichokigundua ni kuwa kuna vijana wengi wamepoteza maisha na kuacha watoto wadogo pamoja wenza. Pia bado kuna familia ambazo hazijapata ndugu zao, na ile miili ambayo haijatambulika teknolojia ya vinasaba inatumika.”

“…kwa wale waliopata majeraha wanaweza kurejea kwenye hali ya kawaida kisaikolojia, lakini kuna tofauti ya uwezo binafsi wa kupona, wengine inaweza kuwachukua muda kidogo. Sisi kwa kipindi cha wiki mbili kazi yetu kubwa ni kuwaunganisha na familia zao na kuwapa msaada wa kiushauri. Na baada ya siku 14 timu ya wataalamu wa mkoa wa Morogoro itaendelea kufuatilia maendeleo yao,” ameeleza Dkt Ng’ondi.

Baadhi ya matukio ya mikasa ya malori ya mafuta Afrika

  • January 31 2009 Kenya: Moto uliwachoma watu waliokuwa wakifyonza mafuta wakati lori la mafuta lilipoanguka huko Molo kaskazini mwa mji wa Nairobi na kuwaoa watu 122.
  • Julai 2, 2010, DR Congo: Takriban watu 292 waliuawa wakati lori la mafuta lilipolipuka mashariki mwa kijiji cha Sange. Baadhi ya waathiriwa walikuwa wakijaribu kuiba mafuta baada ya ajali hiyo huku wengine wakitazama mechi ya kombe la dunia.
  • Oktoba 6, 2018 DR Congo: Takriban watu 53 waliuawa baada ya lori la mafuta kugongana na gari jingine na kushika moto katika barabara kuu ya mji mkuu wa Kinshasa
  • Septemba 16 2015 Sudan Kusini: Watu 203 walifariki na wengine 150 kujeruhiwa wakati watu walipokuwa wakijaribu kuiba mafuta.
  • Novemba 17 2016 Msumbiji: Takriban watu 93 waliuawa wakati lori la mafuta lililokuwa likibeba petroli lilipolipuka magharibi mwa taifa hilo . Mamia walikuwa wakijaribu kufyonza mafuta kutoka katika gari hilo.
  • Julai 12 2012, Nigeria: Takriban watu 104 walifariki walipokuwa wakijaribu kuchukua mafuta kutoka kwa lori la mafuta baada ya kuanguka kusini mwa jimbo la River State.
  • Oktoba 9 2009 , Nigeria: Takriban watu 70 walifariki kusini mashariki mwa jimbo la Anambra baada ya lori la mafuta kulipuka huku moto ikichoma magari kadhaa.Source link

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here